Sunday, 25 September 2016

VITU VYA KULA KABLA NA BAADA YA MAZOEZI

Licha ya mazoezi unayofanya kila siku ni muhimu kufahamu vitu vya kula kabla na baada ya mazoezi hayo, maana vyakula hivyo vina mchango muhimu kwa afaya yako. Kwa ajili  ya kufurahia na kupata faida ya mazoezi hayo ambayo mara nyingi huchukua nguvu nyingi ya mwili ni vizuri kuwa mwangalifu ni kiasi gani cha chakula utatumia. Hakikisha kabla ya mazoezi yoyote unapata kiasi kidogo cha chakula kitakachokufanya uwe na nguvu wakati wa mazoezi ili kuimarisha nguvu ya misuli yako ili uweze kuchoma kalori nyingi na kuboresha afya ya mwili wako bila tabu yoyote.

Hakikisha unakula saa 1-2 kabla ya mazoezi na kisiwe na kalori zaidi ya 300-500 usile chakula mara na kuanza mazoezi. Unaweza ukala ndizi au mkate wa ata (brown bread), oatmeal au viazi vikuu vichache.

Baada ya mazoezi hakikisha unakula baada ya dk 20-60 ili mwili wako uweze kurudisha virutubisho vilivyotoka wakati wa mazoezi, hakikisha unachanganya vyakula vya wanga vyenye afya na protini vyenye kalori 400.
Vyakula hivyo ni kama:-

  • Kuku na wali wa kahawia au (Brown rice)
  • Yai na mkate uliochomwa vizuri
  • Lozi na maziwa mgando
  • Chokoleti zisizo na sukari kwa wingi.

VYAKULA VYA KUVIEPUKA WAKATI UNATAKA KUPUNGUZA UZITO


Katika kipindi cha kupunguza uzito ni kipindi ambacho unatakiwa kuwa makini sana na vyakula unavyokula, maana kama unafanya diet au mazoezi mara nyingi mara baada ya mazoezi mwili unakuwa na uhitaji wa kula sasa hapo ndio pakuwa makini unajaza nini maana badala ya kupunguza uzito unaweza jikuta unaongezeka kutokana na kutokuwa makini na ulaji na aina ya chakula.

Wakati wa kipindi cha kupunguza uzito epuka kunywa soda, juice zenye sukari kwa wingi, vinywaji vyenye kalori kwa wingi . Pia epuka kula mikate mweupe maana haina lishe kama mkate wa ata. Vyakula vingine hatarishi katika zoezi la kupunguza uzito ni vyakula vya migahawani kama burger, chips maana vyakula hivi vina wingi wa mafuta.

VYAKULA 10 VINAVYOWEZA KUONDOA MAFUTA KWENYE TUMBO

Watu wengi husumbuliwa na ukubwa wa matumbo(vitambi) hata wengine kupelekea kutumia dawa mbalimbali zinazoonekana kwenye kila mtandao zenye madai ya kupunguza tumbo. Hili husumbua watu wote wanawake kwa wanaume limekuwa janga duniani kote ni jinsi gani watu wanaweza kuondoa mafuta yanayosababisha ukubwa wa tumbo, imepelekea hata wengine kufanyiwa oparesheni ambazo zinagharimu pesa nyingi. Leo nimejaribu kuonyesha vyakula kumi tu vinavyoweza kuunguza mafuta hayo kwa urahisi bila kutumia pesa nyingi. Hivyo hapo juu vinavyoonekana kwenye picha yetu ni jibu tosha kwa kuyeyusha mafuta ya tumbo.

Thursday, 22 September 2016

VYAKULA VINAVYOWEZA KUPAMBANA NA TATIZO LA CHUNUSI ZA USO

Kama chunusi limekuwa ni tatizo katika ngozi yako basi leo nimekuletea baadhi ya vyakula ambavyo vinaweza kuwa msaada mkubwa kwako katika kupambana na tatizo la chunusi. Baadhi ya vyakula hivyo ni:-

  1.  vyakula ambavyo vina wingi wa Omega 3s, vyakula vyenye wingi wa Omega 3s ni kama mafuta ya samaki, maharag, jozi, samaki, spinach nk.
  2. Maji. Unywaji wa maji kw awingi husaidia kuondoa tatizo la chunusi
  3. Vitunguu Swaumu na Vitunguu maji
  4. Asali safi mbichi
  5. Mdalasini
  6. Mafuta ya nazi, Maziwa na Maji
  7. Nafaka zisizokobolewa na mchele wa rangi ya kahawia
  8. Broccoli
  9. Maharage
  10. Kuku wa aina zote
  11. Mayai 
  12. Vyakula vya bahari kama samaki
  13. Karanga kwa kiasi kdg zitumike
  14. Parachichi
  15. Zabibu nyekundu
  16. Shamari (ni zao liko kwenye jamii ya karoti)
  17. Nyanya
  18. Tikiti maji
  19. Karoti
  20. Viazi vitamu.


Monday, 12 September 2016

SALAD YA UONO KWA AFYA YAKO


JINSI YA KULA KWA AFYA BORA

Ili uweze kuwa na afya bora unaweza kuamua kubadili kutoka kwenye kula vyakula vyeupe na kuhamia kula vyakula vya kahawia. Kama sukari ya kahawia, wali wa kahawia, mkate wa kahawia vyote hivi vinapatikana katika maduka makubwa na madogo.
*ANZA SASA KUJENGA AFYA BORA KWA FAMILIA YAKO*

MAZOEZI MUHIMU KWA KILA ASUBUHI


MATUNDA YENYE KUZUIA MAGONJWA KWA HARAKA

 Kazi ya zabibu ni kuboresha nguvu ya ubongo.
 Pistachio ni nzuri kwa kupambana na mafuta yaliyozidi kwenye damu.
 Aprokoti ni tunda lenye kuweza kupambana na unene uliopitiliza unaosababishwa na ugonjwa wa kisukari.
 Kiwi ni tunda linalosaidia mmeng'enyo mzuri wa chakula.
 Tufaha ni tunda linaloongeza kinga ya mwili au mfumo wa kinga mwilini.
 Korosho ni nzuri kwa kushusha shinikizo la damu.
 Lozi ni nzuri kwa kustawisha mfumo wa neva.
 Tikiti maji linasaidia kazi vizuri katika figo.
 Jozi ni nzuri kuliwa kwa maana zinazuia ugonjwa wa moyo kwa kiasi kikubwa.

KANUNI 7 ZA MAISHA YENYE AFYA BORA

Kuishi bila kuugua ugua hakika inawezekana kama utafwata kanuni hizi. Zipo kanuni nyingi lakini leo nitaelezea kanuni chache tu ili kukuwezesha kuweza kuishi maisha yenye afya bora.
Kanuni ya kwanza ni :-

  • Kunywa maji kwa wingi soda kwa uchache sana
  • Pombe kwa uchache kunywa chai kwa wingi
  • Tumia matunda kwa wingi kuliko kiwango cha pipi
  • Mbogamboga kwa wingi nyama kwa kiwango kidogo
  • Muda mwingi tumia kutembea  kuliko kukaa
  • Hakikisha hupati hasira mara kwa mara badala yake uwe mwenye furaha na kicheko
  • Maneno yawe machache muda mwingi utumike kwa matendo au kazi.

Thursday, 8 September 2016

VITU HATARISHI KWA UBONGO WETU

 Kujifunika kichwa wakati wa kulala . Inaweza ikaonekana kama kitu cha ajabu kwa uhalisia tunahitaji hewa safi hasa wakati wa kulala hii inasababisha kupunguza kiwango cha kupumua hewa safi.
 Uvutaji wa hewa chafu unapelekea kunyima ubongo hewa safi kwavile ubongo unahitaji sana hewa safi ili ufanye kazi vizuri.
 Kiwango kikubwa cha sukari ni chanzo kimojawapo cha uharibifu kwa ubongo.
 Uvutaji sigara unaharibu kwa kiasi kikubwa ubongo na ina madhara mengi mwilini. Kwa madhara katika ubongo inasababisha ubongo kusinyaa na hata kusababisha madhara ya akili 
 Kukosa mawazo mazuri na vichocheo katika mawazo kunaweza pelekea ubongo kusinyaa kwa kutokuutendea kazi.
 Kutokupata kifungua kinywa kila mara inaharibu mfumo wa sukari mwilini na usipokula ubongo hautapata virutubisho na ni rahisi kuharibiwa.
 Kuongea mara chache kunaharibu ubongo. Kwasababu kuongea sana inasababisha ubongo kufanya kazi vizuri na kuuchangamsha.
 Kukosa usingizi kwa muda mrefu inapunguza afya ya seli za ubongo.
Kula kupita kiasi inapelekea uzito kuongezeka na kudidimiza ubongo na kupunguza uwezo wa kufikiri.

VYAKULA UNAVYOWEZA KUCHANGANYA PAMOJA NA VIKAKUPA MATOKEO MAZURI KWA AFYA

 Spinach na limao,mboga za majani zina wingi wa madini ya chuma unapokamulia limao kidogo inasaidia kufyonza madini ya chuma kwa ufanisi zaidi.
 Strwaberries na spinach changanya pamaoja tengeneza salad kama una tatizo la upungufu wa damu kwa mchanganyiko huo wa madini ya chuma kutoka kwa spinach na wingi wa vitamin c kutoka kwenye strwaberries utapata damu kwa wingi.
 Nyanya na mafuta ya mzeituni kwa mchanganyiko huu inasaidia kupunguza kiwango cha mafuta mwilini,shinikizo la damu na ukuaji wa kansa.
 Jibini na yai, mwili unahitaji vitamini D ili kuimarisha mifupa. Kiini cha yai kina vitamin D kwa wingi. Kaanga yai na nyunyizia jibini juu ya yai.
 Mchanganyiko huu wa matunda ya blackberries,blueberries strwaberries na raspberries yakichanganywa pamoja yatakupa lishe ya kutosha sana mwilini.
 Ndizi na maziwa ya mtindi yanafaa kwa kifungua kinywa chako au mara baada ya mazoezi . Ni mchanganyiko wa pottasium inayopatikana kwenye ndizi na protini inayopatikana kweney maziwa mtindi inasaidia kujenga misuli na kujaza amino acid iliyopungua wakati wa mazoezi ya viungo.
Samaki na unga wenye mchanganyiko wa viungo mbalimbali.Samaki ana madini mengi  na shahamu DHA na EPA vikichanganywa vizuri inasaidia kupunguza hatari ya kupata kansa.

ZIFAHAMU FAIDA 10 ZA NDIZI MBIVU MWILINI


Ndizi ni tunda lenye Vitamin C kwa wingi faida nyingi mwilini lakini leo nitazungumzia faida kumi tu.
  1. Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuondoa unyongovu au huzuni.
  2. Ina uwezo wa kurekebisha mfumo wa tumbo
  3. Ina uwezo wa kupunguza shinikizo la damu na hatari ya ugonjwa wa moyo
  4. Inasaidia mifupa kuwa imara kabisa
  5. Kwa mtu mmoja kuna uwezekano wa kupunguza au kuacha uvutaji sigara
  6. Inasaidia kuzuia upungufu wa damu mwilini
  7. Inatupatia nguvu kama italiwa kila mara
  8. Kupunguza maumivu wakati wa hedhi
  9. Kutupa nguvu ya ubongo
  10. Kusaidia kuzuia vidonda vya tumbo.











Banana Nutrition Facts

Serving Size: 3.5 ounces (100 grams), raw
% Daily
Value
*
Amt. Per
Serving
Calories
89
    Calories from fat
3
Total fat
0 g
1%
    Saturated fat
0 g
1%
    Trans fat
Cholesterol
0 mg
0%
Sodium
1 mg
0%
Total Carbohydrate
23 g
8%
    Dietary Fiber
3 g
10%
    Sugar
12 g
Protein
1 g
Vitamin A
1%
Vitamin C
15%
Calcium
1%
Iron
1%
*Percent Daily Values are based on a 2,000 calorie diet. Your daily values may be higher or lower depending on your calorie

VYAKULA NA MATUNDA YANAYOFANANIA NA VIUNGO VYETU VYA MWILI











Wednesday, 7 September 2016

MAAJABU YA KITUNGUU SWAUMU

Kwa kifua na mafua tumia kitunguu swaumu kwa vile ni antibiotic nzuri sana.
Kama una maumivu ya jino saga kitunguu swaumu punje moja changanya na chumvi kidogo na upake kwenye jino bovu acha kwa dakika chache kisha sukutua kwa maji vuguvugu yenye chumvi.
Kwa sehemu ya kidonda kwenye mifupa inayouma au uvimbe sugulia punje ya kitunguu swaumu.
Kwa shida ya kupata usingizi hakikisha unakula salad yenye kitunguu swaumu.
Kama nywele zako zinakatika katika basi kitunguu swaumu ni dawa tosha ya kuzuia nywele kukatika saga kitumguu swaumu upate juice yake ile juisi changanya na chai ya rosemary kijiko kinoja cha asali na juisi ya limao kisha pakaa kichwani kwa dk 15. kisha osha vizuri .
Kwa mishipa ya damu iliyoziba kitunguu swaumu kinasaidia kuzibua na kuboresha mzunguko wa damu.

Tatizo la kuvuta sigara chukua kitunguu swaumu kibichi hakikisha unakila ukiwa hujala kitu chochote kwanza tumbo liwe tupu punje mbili na juisi ya limao kabla ya chakula cha mchana na kabla ya chakula cha usiku punje mbili tu.
Kwa matatizo yote ya kifua waweza pakaa swaumu iliyosagwa kifuani na kuzuia mafua na mzio swaumu changanya na asali na limao utapata matokea mazuri.
Kwa maumivu ya misuli saga swaumu na usugulie kwenye eneo lililodhurika.
Kwa tatizo la visunzua na makovu pakaa kitunguu swaumu kilichomenywa kwenye eneo lenye madoa hasa yaliyosababishwa na chunusi na kwa visunzua paka eneo lenye kisunzua acha kwa dk chache kisha osha.
Kama sikio linauma saga punje 2 zichemshe kisha chuja na uweke matone mwaili ndani ya sikio linalouma.
Kwa matatizo ya ugonjwa wa shinikizo la damu chukua punje 2 changanya sukari, na glasi ya maji upate syrup ili kushusha presha ya kupanda tumia kijiko cha chai  kupimia uwekevijiko 2 vya  mchanganyiko wako .