Monday, 12 September 2016

SALAD YA UONO KWA AFYA YAKO


JINSI YA KULA KWA AFYA BORA

Ili uweze kuwa na afya bora unaweza kuamua kubadili kutoka kwenye kula vyakula vyeupe na kuhamia kula vyakula vya kahawia. Kama sukari ya kahawia, wali wa kahawia, mkate wa kahawia vyote hivi vinapatikana katika maduka makubwa na madogo.
*ANZA SASA KUJENGA AFYA BORA KWA FAMILIA YAKO*

MAZOEZI MUHIMU KWA KILA ASUBUHI


MATUNDA YENYE KUZUIA MAGONJWA KWA HARAKA

 Kazi ya zabibu ni kuboresha nguvu ya ubongo.
 Pistachio ni nzuri kwa kupambana na mafuta yaliyozidi kwenye damu.
 Aprokoti ni tunda lenye kuweza kupambana na unene uliopitiliza unaosababishwa na ugonjwa wa kisukari.
 Kiwi ni tunda linalosaidia mmeng'enyo mzuri wa chakula.
 Tufaha ni tunda linaloongeza kinga ya mwili au mfumo wa kinga mwilini.
 Korosho ni nzuri kwa kushusha shinikizo la damu.
 Lozi ni nzuri kwa kustawisha mfumo wa neva.
 Tikiti maji linasaidia kazi vizuri katika figo.
 Jozi ni nzuri kuliwa kwa maana zinazuia ugonjwa wa moyo kwa kiasi kikubwa.

KANUNI 7 ZA MAISHA YENYE AFYA BORA

Kuishi bila kuugua ugua hakika inawezekana kama utafwata kanuni hizi. Zipo kanuni nyingi lakini leo nitaelezea kanuni chache tu ili kukuwezesha kuweza kuishi maisha yenye afya bora.
Kanuni ya kwanza ni :-

  • Kunywa maji kwa wingi soda kwa uchache sana
  • Pombe kwa uchache kunywa chai kwa wingi
  • Tumia matunda kwa wingi kuliko kiwango cha pipi
  • Mbogamboga kwa wingi nyama kwa kiwango kidogo
  • Muda mwingi tumia kutembea  kuliko kukaa
  • Hakikisha hupati hasira mara kwa mara badala yake uwe mwenye furaha na kicheko
  • Maneno yawe machache muda mwingi utumike kwa matendo au kazi.