Thursday, 8 September 2016

VITU HATARISHI KWA UBONGO WETU

 Kujifunika kichwa wakati wa kulala . Inaweza ikaonekana kama kitu cha ajabu kwa uhalisia tunahitaji hewa safi hasa wakati wa kulala hii inasababisha kupunguza kiwango cha kupumua hewa safi.
 Uvutaji wa hewa chafu unapelekea kunyima ubongo hewa safi kwavile ubongo unahitaji sana hewa safi ili ufanye kazi vizuri.
 Kiwango kikubwa cha sukari ni chanzo kimojawapo cha uharibifu kwa ubongo.
 Uvutaji sigara unaharibu kwa kiasi kikubwa ubongo na ina madhara mengi mwilini. Kwa madhara katika ubongo inasababisha ubongo kusinyaa na hata kusababisha madhara ya akili 
 Kukosa mawazo mazuri na vichocheo katika mawazo kunaweza pelekea ubongo kusinyaa kwa kutokuutendea kazi.
 Kutokupata kifungua kinywa kila mara inaharibu mfumo wa sukari mwilini na usipokula ubongo hautapata virutubisho na ni rahisi kuharibiwa.
 Kuongea mara chache kunaharibu ubongo. Kwasababu kuongea sana inasababisha ubongo kufanya kazi vizuri na kuuchangamsha.
 Kukosa usingizi kwa muda mrefu inapunguza afya ya seli za ubongo.
Kula kupita kiasi inapelekea uzito kuongezeka na kudidimiza ubongo na kupunguza uwezo wa kufikiri.

No comments:

Post a Comment