THIS IS AN EXCEPTIONAL BLOG FOR ANYONE ASPIRING TOWARDS IMPROVED HEALTH AND EXCELLENT BODY FITNESS.
IT OFFER ALL KINDS OF POPULAR GYM EXERCISES INCLUDING AEROBIC,BODY BUILDING ETC
Karibu katika kipengele hiki cha Recipes tutakuwa tukiongelea jinsi ya kutengeneza juisi za aina mbalimbali zenye faida katika miili yetu pamoja na vyakula vyenye afya na kujenga miili yetu. Leo tutaanza na juisi za kulinda mifupa yetu. Karibuni!!!
Hii ni juisi ya tufaha na chungwa ni maalum kwa ajili ya watoto hii inasaidia kuwapa nguvu.
Tufaha 1-2 na chungwa au machungwa mawili
saga tufaha kisha chuja na baada ya hapo kamua machungwa yako kisha changanya mchanganyiko wa juisi ya tufaha na maji ya machungwa pamoja.Koroga vizuri mpatie mtoto aburudike nayo.
MAHITAJI :-
Matufaha (Apples) 4 za rangi ya kijani
Figiri miche yake kata majani yote tumia vijiti 3 urefu wa '11-12' inch
Mchicha ua mboga ya jamii ya mchicha fungu 2
Limao 1
Saga kwenye blender vyote kisha chuja iache ipoe kwenye jokofu( fridge) kwa muda wa lisaa limoja kamulia limao lako na itakuwa tayari kwa kunywewa hakikisha una itikisa vizuri, ni nzuri sana katika kuboresha mifupa na ina faida nyingi nyingi tu.
Kabichi nyekundu robo
Matufaha 4 (apples) ya rangi nyekundu
Ndimu moja
Saga vyote kwenye blender na upate juisi ya rangi hii. Juisi hii inasaidia sana kuimarisha mifupa, kupambana na kansa, na inasaidia usagaji mzuri wa chakula mwilini.
No comments:
Post a Comment