Friday, 26 August 2016

BAADHI YA VITU VYA KUEPUKA KWA AFYA ZA WATOTO


Ni muhimu sana kwa wazazi na walezi kuangalia ni vitu gani tunawapa watoto. Vyakula visivyokuwa sahihi ni hatari kwa afya na makuzi ya watoto.

AFYA BORA NI KILA KITU KATIKA MAISHA


MATUNDA NA MBOGA MBOGA ZINAZOSAIDIA KUPUNGUZA UZITO AMA KUONGEZA UZITO

Wakati wengi wanafanya kila juhudi kupunguza uzito wapo pia wanatamani kuongeza uzito. Nikaona sio vibaya nikiweka chati hii ili kama uko kwenye kundi la kupunguza uzito ujue ni matunda gani na mboga gani zinafaa katika safari ya kupunguza uzito na kwa wale wanaotaka kuongeza uzito vivyo hivyo.




KIWANGO CHA MAJI UNACHOTAKIWA KUNYWA ILI KUPUNGUZA UZITO KUTOKANA NA MWILI WAKO



Maji ni uhai katika mwili wa mwanadamu, lakini pia maji ni muhimu kwa afya na urembo. Unywaji wa maji mengi unasaidia kukupa mwonekano mzuri wa ngozi,kupunguza mwili, kuwa na afya na kukufanya mwenye nguvu. Watu wengi hawajui umuhimu wa maji katika mwili. Kwa wale wanaotaka kupunguza uzito kwa haraka inawapasa kunywa maji mengi . Utafiti unaonyesha kuwa kama unataka kupunguza uzito hakikisha unakunywa glass 2 za maji kabla ya kula hii itapelekea tumbo kujaa na wewe kula chakula kidogo.
Kwa wale wanataka kupunguza uzito hakikisha unajua uzito wako kabla ya kunywa maji ili uweze kuelewa ni kiwango gani cha maji unatakiwa kunywa ili kupunguza uzito wako.
Asubuhi kabla ya kitu chochote hakikisha unakunywa maji.


KUNYWA MAJI KWA AFYA BORA. 

VITU 15 AMBAVYO NI LAZIMA UACHE KUVIAMINI KUHUSIANA NA MILO YENYE AFYA

Hivi sasa kumekuwa na mijadala mingi kuhusiana na milo iletayo afya bora na kuna maoni tofauti tofauti ya jinsi gani ya kula, wakati gani wa kula, nini cha kula, na kiasi gani cha chakula cha kula. Baadhi ya mapendekezo yamekuwa yakitiliwa mashaka na watafiti mbalimbali. Brightside wakaamua kufanya utafiti na kuja na mapendekezo haya niliyoshare  kwenye blog hii kama ifuatavyo:-