Saturday, 1 October 2016

PATA MUONEKANO MZURI WENYE KUVUTIA

Hakika hakuna mtu asiyependa kuwa na muonekano mzuri wa kuvutia. ila muonekano mzuri haupatikani tu hivi hivi hakuna kizuri kisicho na gharama. Gharama ya kuwa na muonekano mzuri na wenye kuvutia ni kula vizuri, kuwa na afya bora, kula kwa kuzingatia kanuni za afya, kufanya mazoezi nk.
Kwa kula matunda na mbogamboga ni sehemu ya kujipatia afya bora na si bora afya. Lakini kwa kuepuka kula vyakula visivyo na tija katika miili yetu hakika tutapata afya njema. Katika picha hii ni baadhi ya vyakula ambavyo ukivitumia mara kwa mara kwa familia yako utajenga familia yenye afya bora isiyokuwa na magonjwa yatokanayo na kula bila mpangilio.

  • AFYA NI KILA KITU KATIKA MAISHA YAKO HAKIKISHA UNAILINDA KWA KULA VIZURI