Wednesday, 7 September 2016

MAAJABU YA KITUNGUU SWAUMU

Kwa kifua na mafua tumia kitunguu swaumu kwa vile ni antibiotic nzuri sana.
Kama una maumivu ya jino saga kitunguu swaumu punje moja changanya na chumvi kidogo na upake kwenye jino bovu acha kwa dakika chache kisha sukutua kwa maji vuguvugu yenye chumvi.
Kwa sehemu ya kidonda kwenye mifupa inayouma au uvimbe sugulia punje ya kitunguu swaumu.
Kwa shida ya kupata usingizi hakikisha unakula salad yenye kitunguu swaumu.
Kama nywele zako zinakatika katika basi kitunguu swaumu ni dawa tosha ya kuzuia nywele kukatika saga kitumguu swaumu upate juice yake ile juisi changanya na chai ya rosemary kijiko kinoja cha asali na juisi ya limao kisha pakaa kichwani kwa dk 15. kisha osha vizuri .
Kwa mishipa ya damu iliyoziba kitunguu swaumu kinasaidia kuzibua na kuboresha mzunguko wa damu.

Tatizo la kuvuta sigara chukua kitunguu swaumu kibichi hakikisha unakila ukiwa hujala kitu chochote kwanza tumbo liwe tupu punje mbili na juisi ya limao kabla ya chakula cha mchana na kabla ya chakula cha usiku punje mbili tu.
Kwa matatizo yote ya kifua waweza pakaa swaumu iliyosagwa kifuani na kuzuia mafua na mzio swaumu changanya na asali na limao utapata matokea mazuri.
Kwa maumivu ya misuli saga swaumu na usugulie kwenye eneo lililodhurika.
Kwa tatizo la visunzua na makovu pakaa kitunguu swaumu kilichomenywa kwenye eneo lenye madoa hasa yaliyosababishwa na chunusi na kwa visunzua paka eneo lenye kisunzua acha kwa dk chache kisha osha.
Kama sikio linauma saga punje 2 zichemshe kisha chuja na uweke matone mwaili ndani ya sikio linalouma.
Kwa matatizo ya ugonjwa wa shinikizo la damu chukua punje 2 changanya sukari, na glasi ya maji upate syrup ili kushusha presha ya kupanda tumia kijiko cha chai  kupimia uwekevijiko 2 vya  mchanganyiko wako .

No comments:

Post a Comment