Tunda hili la tende au dates kwa huota sana kwenye maeneo ya jangwa na yenye joto na ardhi kavu isiyotunza maji, yanastawi kwa wingi katika nchi za mashariki ya kati.
Leo nitaongelea sababu kumi kati ya nyingi za kwanini tutumie tunda la tende, Sababu hizo ni kama ifuatavyo:-
- Huongeza nguvu mwilini kutokana na kuwa na sukari ya asili, pia waweza
- tengeneza juisi ya maziwa na tende
- Huzuia meno kuoza pia ni tiba kwa wagonjwa wa anemia kutokana na kuwa na madini mengi ya chuma
- Kutokana na kuwa na vitamini na madini kwa wingi hupunguza uwezekano wa kupata kiharusi
- Huongeza uwezo wa kujamiiana kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha nguvu
- Unaweza kutumia kama mbadala wa sukari
- Kwa wajawazito , humuongezea nguvu mama
- Huimarisha mifupa kutokana na kuwa na wingi wa madini ya chuma, potassium kwa wingi
- Kutokana na kuwa na kamba kamba husaidia mtu kupata choo kilaini na kwa urahisi
- Hongeza mwili kwa haraka kwa wale waliokonda hivyo kama huitaji kuongeza mwili usitumie tende kwa kila wakati
- Kwa wenye matatizo ya upungufu wa madini ya chuma tende inasaidia kuongeza madini ya chuma kwa kiwango kikubwa.
**Hizi ni baadhi kati ya sababu nyingi na faida nyingi za kula tende *.