Sunday, 25 September 2016

VITU VYA KULA KABLA NA BAADA YA MAZOEZI

Licha ya mazoezi unayofanya kila siku ni muhimu kufahamu vitu vya kula kabla na baada ya mazoezi hayo, maana vyakula hivyo vina mchango muhimu kwa afaya yako. Kwa ajili  ya kufurahia na kupata faida ya mazoezi hayo ambayo mara nyingi huchukua nguvu nyingi ya mwili ni vizuri kuwa mwangalifu ni kiasi gani cha chakula utatumia. Hakikisha kabla ya mazoezi yoyote unapata kiasi kidogo cha chakula kitakachokufanya uwe na nguvu wakati wa mazoezi ili kuimarisha nguvu ya misuli yako ili uweze kuchoma kalori nyingi na kuboresha afya ya mwili wako bila tabu yoyote.

Hakikisha unakula saa 1-2 kabla ya mazoezi na kisiwe na kalori zaidi ya 300-500 usile chakula mara na kuanza mazoezi. Unaweza ukala ndizi au mkate wa ata (brown bread), oatmeal au viazi vikuu vichache.

Baada ya mazoezi hakikisha unakula baada ya dk 20-60 ili mwili wako uweze kurudisha virutubisho vilivyotoka wakati wa mazoezi, hakikisha unachanganya vyakula vya wanga vyenye afya na protini vyenye kalori 400.
Vyakula hivyo ni kama:-

  • Kuku na wali wa kahawia au (Brown rice)
  • Yai na mkate uliochomwa vizuri
  • Lozi na maziwa mgando
  • Chokoleti zisizo na sukari kwa wingi.

VYAKULA VYA KUVIEPUKA WAKATI UNATAKA KUPUNGUZA UZITO


Katika kipindi cha kupunguza uzito ni kipindi ambacho unatakiwa kuwa makini sana na vyakula unavyokula, maana kama unafanya diet au mazoezi mara nyingi mara baada ya mazoezi mwili unakuwa na uhitaji wa kula sasa hapo ndio pakuwa makini unajaza nini maana badala ya kupunguza uzito unaweza jikuta unaongezeka kutokana na kutokuwa makini na ulaji na aina ya chakula.

Wakati wa kipindi cha kupunguza uzito epuka kunywa soda, juice zenye sukari kwa wingi, vinywaji vyenye kalori kwa wingi . Pia epuka kula mikate mweupe maana haina lishe kama mkate wa ata. Vyakula vingine hatarishi katika zoezi la kupunguza uzito ni vyakula vya migahawani kama burger, chips maana vyakula hivi vina wingi wa mafuta.

VYAKULA 10 VINAVYOWEZA KUONDOA MAFUTA KWENYE TUMBO

Watu wengi husumbuliwa na ukubwa wa matumbo(vitambi) hata wengine kupelekea kutumia dawa mbalimbali zinazoonekana kwenye kila mtandao zenye madai ya kupunguza tumbo. Hili husumbua watu wote wanawake kwa wanaume limekuwa janga duniani kote ni jinsi gani watu wanaweza kuondoa mafuta yanayosababisha ukubwa wa tumbo, imepelekea hata wengine kufanyiwa oparesheni ambazo zinagharimu pesa nyingi. Leo nimejaribu kuonyesha vyakula kumi tu vinavyoweza kuunguza mafuta hayo kwa urahisi bila kutumia pesa nyingi. Hivyo hapo juu vinavyoonekana kwenye picha yetu ni jibu tosha kwa kuyeyusha mafuta ya tumbo.