Wednesday, 24 August 2016

VYAKULA VYA ASILI VYENYE UWEZO WA KUREJESHA NGUVU ZA KIUME

 Upungufu wa nguvu za kiume ni nini? ni mwanaume kutokuwa na uwezo wa kutoa mbegu bora zenye uwezo wa kutungisha mimba au kusimama kwa uume.
Ndoa nyingi hivi sasa zimekumbwa na tatizo la wanaume kukosa nguvu za kiume, takwimu zilizopo zinaonyesha zaidi ya asilimia 60 ya wanandoa wanakabiliwa na tatizo hili.
Kutokana na matatizo haya watu wengi wamejikuta wakiangukia kwenye dawa zisizofaa na kusababisha madhara zaidi na hadi kupelekea vifo.
Matatizo haya huchangiwa na kuugua kwa muda mrefu, kisukari,na mionzi ya simu. Pia dawa za kuulia wadudu zinaweza sababisha tatizo hili kutokana na kuwa na viambata sumu iitwayo estrogen, matatizo ya kisaikolojia na hata upigaji punyeto kwa muda mrefu na uulaji wa vyakula vyenye kemikali.

Kuna aina mbili ya viungo na matunda ambayo yamefanyiwa utafiti na kubainika kuongeza nguvu ya kiume na hakuna madhara katika uongezaji wa nguvu za kiume katika vitu hivyo vyenye uwezo wa kuongeza nguvu za kiume kwa njia ya asili ni:-

TANGAWIZI


Tangawizi ni moja ya kiungo kinachoweza kurejesha nguvu za kiume, unaweza kuichemsha tangawizi na utaitumia kuinywa kama chai asubuhi, mchana na jioni. Pia tangawizi unaweza kuichanganya na habat soda,asali, kitunguu swaumu na tangawizi yenyewe.

JINSI YA KUTUMIA MCHANGANYIKO HUU
Chukua kitunguu swaumu na tangawizi vitwange kisha vichanganye na asali pamoja na habat soda na uwe unakunywa mchanganyiko huu kwa kutumia kijiko cha chai kutwa mara 3 kwa muda wa wiki moja na utaona mabadiliko.

TIKITI MAJI


Tunda hili nalo linasaidia kuongeza nguvu za kiume waweza kulila lenyewe au ukasaga juisi na kuinywa kila siku.

MAAJABU YA MAJANI YA MPERA KWA UREMBO NA AFYA



Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla
Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium.

FAIDA 16 MUHIMU ZITOKANAZO NA MAJANI YA MPERA

  1. Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua na kikohozi
  2. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio (allergy)
  3. Pia majani haya ya mpera yakichemshwa kama chai yanaondoa cholesterol iliyozidi mwilini
  4. Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango cha tatizo la sukari mwilini
  5. Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume
  6. Pia inatumika kama scrub ya uso chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi na inasaidia kuondoa uchafu usoni
  7. Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawa ya kuponyesha tumbo la kuhara
  8. Kama umejikata kidogo unaweza kutumia majani ya mpera yalioshwa na kusagwa vizuri kwa kupunguza maumivu na kukulinda na maambukizi ya bakteria
  9. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu eneo la mwili lililong'atwa na mdudu na kupunguza maumivu
  10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa ina uwezo wa kutibu tezi dume
  11. Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingi majani ya mpera yana uwezo mkubwa wa kutibu chunusi
  12. Chai ya majani ya mpera inasaidia kupunguza uzito mwilini na kuzuia uharibifu ndani ya sukari mwilini
  13. Majani ya mpera yanajaza nywele na kurefusha nywele kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele, unasaga na kuchemsha kisha acha yapoe ndio upake kichwani kutoka chini ya ngozi ya kichwa hadi kwenye ncha ya nywele zako
  14. Ukiwa na tatizo la vidonda kwenye ufizi, maumivu ya jino na ufizi tafuna majani ya mpera na utaona maajabu ya majani haya
  15. Chukua majani ya mpera saga vizuri mpaka yawe laini kabisa ongeza na maji kidogo kisha tumia kupaka usoni kama scrub inatibu ngozi inayoonza kuzeeka mapema
  16. Chai ya mpera inasaidia kwa kutibu mvurugiko wa tumbo.