Wednesday, 24 August 2016

MAAJABU YA MAJANI YA MPERA KWA UREMBO NA AFYA



Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla
Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium.

FAIDA 16 MUHIMU ZITOKANAZO NA MAJANI YA MPERA

  1. Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua na kikohozi
  2. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio (allergy)
  3. Pia majani haya ya mpera yakichemshwa kama chai yanaondoa cholesterol iliyozidi mwilini
  4. Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango cha tatizo la sukari mwilini
  5. Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume
  6. Pia inatumika kama scrub ya uso chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi na inasaidia kuondoa uchafu usoni
  7. Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawa ya kuponyesha tumbo la kuhara
  8. Kama umejikata kidogo unaweza kutumia majani ya mpera yalioshwa na kusagwa vizuri kwa kupunguza maumivu na kukulinda na maambukizi ya bakteria
  9. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu eneo la mwili lililong'atwa na mdudu na kupunguza maumivu
  10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa ina uwezo wa kutibu tezi dume
  11. Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingi majani ya mpera yana uwezo mkubwa wa kutibu chunusi
  12. Chai ya majani ya mpera inasaidia kupunguza uzito mwilini na kuzuia uharibifu ndani ya sukari mwilini
  13. Majani ya mpera yanajaza nywele na kurefusha nywele kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele, unasaga na kuchemsha kisha acha yapoe ndio upake kichwani kutoka chini ya ngozi ya kichwa hadi kwenye ncha ya nywele zako
  14. Ukiwa na tatizo la vidonda kwenye ufizi, maumivu ya jino na ufizi tafuna majani ya mpera na utaona maajabu ya majani haya
  15. Chukua majani ya mpera saga vizuri mpaka yawe laini kabisa ongeza na maji kidogo kisha tumia kupaka usoni kama scrub inatibu ngozi inayoonza kuzeeka mapema
  16. Chai ya mpera inasaidia kwa kutibu mvurugiko wa tumbo.


No comments:

Post a Comment