GEORGE ADOLF WORKOUT
THIS IS AN EXCEPTIONAL BLOG FOR ANYONE ASPIRING TOWARDS IMPROVED HEALTH AND EXCELLENT BODY FITNESS. IT OFFER ALL KINDS OF POPULAR GYM EXERCISES INCLUDING AEROBIC,BODY BUILDING ETC
Thursday, 19 January 2017
Wednesday, 23 November 2016
KULA SALAD NI MUHIMU KWA AFYA
Salad ni muhimu sana katika mwili kwavile ina wingi wa fiber, fiber hupigana na lehamu mwilini. Fiber iliyoko kwenye salad inasababisha kushiba haraka na kula kidogo hivyo kwa wale wanaopenda kupunguza mwili hii husaidia sana. Salad huanza kuliwa kabla ya chakula kikuu ( main meal). Kula salad kila mara huleta afya kwa wale wasiopenda kuongeza uzito wa mwili.
Na kuna aina mbalimbali za salad inategemea ni ipi unapendelea.
Salad nzuri huleta fat nzuri mwilini, mafuta hayo yanapatikana kwa kuweka parachichi kwa wingi, olive oil katika salad yako husaidia mwili kufyonza phytochemicals nzuri inayotakiwa mwilini. Na salad haina gharama na haihitaji kutengeneza kwa muda mrefu.
KULA SALAD NI MUHIMU KWA AFYA.
Thursday, 10 November 2016
Wednesday, 12 October 2016
FAIDA ZA KUTUMIA TUNDA TENDE MWILINI
Tunda hili la tende au dates kwa huota sana kwenye maeneo ya jangwa na yenye joto na ardhi kavu isiyotunza maji, yanastawi kwa wingi katika nchi za mashariki ya kati.
Leo nitaongelea sababu kumi kati ya nyingi za kwanini tutumie tunda la tende, Sababu hizo ni kama ifuatavyo:-
- Huongeza nguvu mwilini kutokana na kuwa na sukari ya asili, pia waweza
- tengeneza juisi ya maziwa na tende
- Huzuia meno kuoza pia ni tiba kwa wagonjwa wa anemia kutokana na kuwa na madini mengi ya chuma
- Kutokana na kuwa na vitamini na madini kwa wingi hupunguza uwezekano wa kupata kiharusi
- Huongeza uwezo wa kujamiiana kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha nguvu
- Unaweza kutumia kama mbadala wa sukari
- Kwa wajawazito , humuongezea nguvu mama
- Huimarisha mifupa kutokana na kuwa na wingi wa madini ya chuma, potassium kwa wingi
- Kutokana na kuwa na kamba kamba husaidia mtu kupata choo kilaini na kwa urahisi
- Hongeza mwili kwa haraka kwa wale waliokonda hivyo kama huitaji kuongeza mwili usitumie tende kwa kila wakati
- Kwa wenye matatizo ya upungufu wa madini ya chuma tende inasaidia kuongeza madini ya chuma kwa kiwango kikubwa.
**Hizi ni baadhi kati ya sababu nyingi na faida nyingi za kula tende *.
Sunday, 2 October 2016
PAMBANA NA KANSA KWA KUTUMIA VIUNGO HIVI
Kansa au kwa jina lingine unajulikana kama saratani umekuwa ugonjwa unaotesa watu wengi duniani ,kansa kwa kawaida husababishia mwili madhara mengi maana hushambulia tishu za mwili kutokana na kuunda vimbe ( tumor )mbalimbali kwenye mwili. Ila kwa upande wa kansa ya damu ni tofauti maana hapa huzuia utendaji wa kawaida wa damu na kuzifanya seli ziwe na mgawanyiko usio wa kawaida katika damu. Lakini unaweza pamban na kansa kwa kutumia viungo chakula hivi.
UNASUMBULIWA NA MAFUA?
Mafua yamekuwa yakimpata karibia kila mtu ila kuna baadhi ya watu hupatwa na tatizo la mafua mara kwa mara, hivyo basi kama unaona unasumbuliwa mara kwa mara suluhisho lake ni kuhakikisha unakula kitunguu kibichi mara kwa mara kwa maana katika kitunguu kuna Vitamin C, fiber, sulfur na virutubisho vinginevyo.
- USISUMBUKE TENA PONA MAFUA KWA HARAKA KWA KUTAFUNA KITUNGUU KIBICHI!!!
Saturday, 1 October 2016
PATA MUONEKANO MZURI WENYE KUVUTIA
Hakika hakuna mtu asiyependa kuwa na muonekano mzuri wa kuvutia. ila muonekano mzuri haupatikani tu hivi hivi hakuna kizuri kisicho na gharama. Gharama ya kuwa na muonekano mzuri na wenye kuvutia ni kula vizuri, kuwa na afya bora, kula kwa kuzingatia kanuni za afya, kufanya mazoezi nk.
Kwa kula matunda na mbogamboga ni sehemu ya kujipatia afya bora na si bora afya. Lakini kwa kuepuka kula vyakula visivyo na tija katika miili yetu hakika tutapata afya njema. Katika picha hii ni baadhi ya vyakula ambavyo ukivitumia mara kwa mara kwa familia yako utajenga familia yenye afya bora isiyokuwa na magonjwa yatokanayo na kula bila mpangilio.
- AFYA NI KILA KITU KATIKA MAISHA YAKO HAKIKISHA UNAILINDA KWA KULA VIZURI
Sunday, 25 September 2016
VITU VYA KULA KABLA NA BAADA YA MAZOEZI
Licha ya mazoezi unayofanya kila siku ni muhimu kufahamu vitu vya kula kabla na baada ya mazoezi hayo, maana vyakula hivyo vina mchango muhimu kwa afaya yako. Kwa ajili ya kufurahia na kupata faida ya mazoezi hayo ambayo mara nyingi huchukua nguvu nyingi ya mwili ni vizuri kuwa mwangalifu ni kiasi gani cha chakula utatumia. Hakikisha kabla ya mazoezi yoyote unapata kiasi kidogo cha chakula kitakachokufanya uwe na nguvu wakati wa mazoezi ili kuimarisha nguvu ya misuli yako ili uweze kuchoma kalori nyingi na kuboresha afya ya mwili wako bila tabu yoyote.
Hakikisha unakula saa 1-2 kabla ya mazoezi na kisiwe na kalori zaidi ya 300-500 usile chakula mara na kuanza mazoezi. Unaweza ukala ndizi au mkate wa ata (brown bread), oatmeal au viazi vikuu vichache.
Baada ya mazoezi hakikisha unakula baada ya dk 20-60 ili mwili wako uweze kurudisha virutubisho vilivyotoka wakati wa mazoezi, hakikisha unachanganya vyakula vya wanga vyenye afya na protini vyenye kalori 400.
Vyakula hivyo ni kama:-
Hakikisha unakula saa 1-2 kabla ya mazoezi na kisiwe na kalori zaidi ya 300-500 usile chakula mara na kuanza mazoezi. Unaweza ukala ndizi au mkate wa ata (brown bread), oatmeal au viazi vikuu vichache.
Baada ya mazoezi hakikisha unakula baada ya dk 20-60 ili mwili wako uweze kurudisha virutubisho vilivyotoka wakati wa mazoezi, hakikisha unachanganya vyakula vya wanga vyenye afya na protini vyenye kalori 400.
Vyakula hivyo ni kama:-
- Kuku na wali wa kahawia au (Brown rice)
- Yai na mkate uliochomwa vizuri
- Lozi na maziwa mgando
- Chokoleti zisizo na sukari kwa wingi.
Subscribe to:
Posts (Atom)