Wednesday, 12 October 2016

FAIDA ZA KUTUMIA TUNDA TENDE MWILINI



 Tunda hili la tende au dates kwa  huota sana kwenye maeneo ya jangwa na yenye joto na ardhi kavu isiyotunza maji, yanastawi kwa wingi katika nchi za mashariki ya kati.



Tende ni tunda lenye virutubisho katika mwili na lina faida nyingi sana, lina kiwango cha sukari asili asilimia 60-70, sukari hii haileti madhara ya kisukari kama inavyoaminiwa na wengi

Leo nitaongelea sababu kumi kati ya nyingi za kwanini tutumie tunda la tende, Sababu hizo ni kama ifuatavyo:-

  1. Huongeza nguvu mwilini kutokana na kuwa na sukari ya asili, pia waweza 
  2. tengeneza juisi ya maziwa na tende
  3. Huzuia meno kuoza pia ni tiba kwa wagonjwa wa anemia kutokana na kuwa na madini mengi ya chuma
  4. Kutokana na kuwa na vitamini na madini kwa wingi hupunguza uwezekano wa kupata kiharusi
  5. Huongeza uwezo wa kujamiiana kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha nguvu
  6. Unaweza kutumia kama mbadala wa sukari
  7. Kwa wajawazito , humuongezea nguvu mama 
  8. Huimarisha mifupa kutokana na kuwa na wingi wa madini ya chuma, potassium kwa wingi
  9. Kutokana na kuwa na kamba kamba husaidia mtu kupata choo kilaini na kwa urahisi
  10. Hongeza mwili kwa haraka kwa wale waliokonda hivyo kama huitaji kuongeza mwili usitumie tende kwa kila wakati
  11. Kwa wenye matatizo ya upungufu wa madini ya chuma tende inasaidia kuongeza madini ya chuma kwa kiwango kikubwa.




    **Hizi ni baadhi kati ya sababu nyingi na faida nyingi za kula tende *.

    Sunday, 2 October 2016

    PAMBANA NA KANSA KWA KUTUMIA VIUNGO HIVI

    Kansa au kwa jina lingine unajulikana kama saratani umekuwa ugonjwa unaotesa watu wengi duniani ,kansa kwa kawaida husababishia mwili madhara mengi maana hushambulia tishu za mwili kutokana na kuunda vimbe ( tumor )mbalimbali kwenye mwili. Ila kwa upande wa kansa ya damu ni tofauti maana hapa huzuia utendaji wa kawaida wa damu na kuzifanya seli ziwe na mgawanyiko usio wa kawaida katika damu. Lakini unaweza pamban na kansa kwa kutumia viungo chakula hivi.


    • Kitunguu swaumu
    • Tangawizi
    • Mdalasini
    • Binzari
    • Pilipili


    • UNASUMBULIWA NA MAFUA?

      Mafua yamekuwa yakimpata karibia kila mtu ila kuna baadhi ya watu hupatwa na tatizo la mafua mara kwa mara, hivyo basi kama unaona unasumbuliwa mara kwa mara suluhisho lake ni kuhakikisha unakula kitunguu kibichi mara kwa mara kwa maana katika kitunguu kuna Vitamin C, fiber, sulfur na virutubisho vinginevyo.


      • USISUMBUKE TENA PONA MAFUA KWA HARAKA KWA KUTAFUNA KITUNGUU KIBICHI!!!

      Saturday, 1 October 2016

      PATA MUONEKANO MZURI WENYE KUVUTIA

      Hakika hakuna mtu asiyependa kuwa na muonekano mzuri wa kuvutia. ila muonekano mzuri haupatikani tu hivi hivi hakuna kizuri kisicho na gharama. Gharama ya kuwa na muonekano mzuri na wenye kuvutia ni kula vizuri, kuwa na afya bora, kula kwa kuzingatia kanuni za afya, kufanya mazoezi nk.
      Kwa kula matunda na mbogamboga ni sehemu ya kujipatia afya bora na si bora afya. Lakini kwa kuepuka kula vyakula visivyo na tija katika miili yetu hakika tutapata afya njema. Katika picha hii ni baadhi ya vyakula ambavyo ukivitumia mara kwa mara kwa familia yako utajenga familia yenye afya bora isiyokuwa na magonjwa yatokanayo na kula bila mpangilio.

      • AFYA NI KILA KITU KATIKA MAISHA YAKO HAKIKISHA UNAILINDA KWA KULA VIZURI