Wednesday, 23 November 2016

KULA SALAD NI MUHIMU KWA AFYA


Salad ni muhimu sana katika mwili kwavile ina wingi wa fiber, fiber hupigana na lehamu mwilini. Fiber iliyoko kwenye salad inasababisha kushiba haraka na kula kidogo hivyo kwa wale wanaopenda kupunguza mwili hii husaidia sana. Salad huanza kuliwa kabla ya chakula kikuu  ( main meal). Kula salad kila mara huleta afya kwa wale wasiopenda kuongeza uzito wa mwili. 

 Antioxidant mara kwa mara ukila salad unapata kiwango cha juu cha damu kwavile ya mboga mboga na mboga ina antioxidants kwa wingi na muhimu kama vitamin C,Lycopene, beta carotene na folic acid, antioxidants ina sifa ya kulinda ngozi dhidi ya uzee au kuzeeka.
Na kuna aina mbalimbali za salad inategemea ni ipi unapendelea.
Salad nzuri huleta fat nzuri mwilini, mafuta hayo yanapatikana kwa kuweka parachichi kwa wingi, olive oil katika salad yako husaidia mwili kufyonza phytochemicals nzuri inayotakiwa mwilini. Na salad haina gharama na haihitaji kutengeneza kwa muda mrefu.



KULA SALAD NI MUHIMU KWA AFYA.